Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2018

NGUVU YA HEKIMA

Habari za asubuhi! Umeamshwaje! Na ndugu hapo wanaendeleaje? Mithali 24:3-4 [3]Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, [4]Na kwarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Roho wa Mungu akuangazie na kukupatia hekima kuyajenga yale yote yaliowekwa mikononi na moyoni mwako, ufahamu wake ulioko ndani yako ukathibitike na kwa maarifa yake akujaze na kuongeza thamani katika yote. Umebarikiwa. Shalom.

PENDO LA MUNGU

Wakolosai 1:12-13 [12]mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. [13]Nayetuokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; Mungu amethibitisha pendo lake kwako kupitia Kristo Yesu yeye aliye tustahilisha hata sasa kuyatenda yote yalio mbele zetu tukiwa na tumaini jema na mafanikio. Wewe ni wathamani.

WEWE NI WATHAMANI NDANI YA KRISTO

WEWE NI WATHAMANI NDANI YA KRISTO Waefeso 2:5-6 [5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja nKristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. [6]Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; Usisahau yaka umeketishwa pamoja na Kristo Yesu kwa ile imani uliyokuwa nayo ya Kumkiri Kristo Yesu ndani yako kuwa yeye ni Bwana na mokozi wa maisha yako. Shalom.

KUMTIZAMIA KRISTO YESU

KUMTIZAMIA KRISTO YESU. Waefeso 1:17 [17]Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; Ninakuombea Roho Mtakatifu akupe ufunuo kila unapojifunza kwa neno lake uweze kumfuata Kristo Yesu kwakua kila kitu kimewekwa chini yake. Siku yako ni njema.

UNAO UZIMA WA MILELE

UNAO UZIMA WA MILELE 1 Yohana 5:13 [13]Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jinla Mwana wa Mungu. ninakuombea Roho wa Mungu akufunulie kweli hii na Utukufu wa Mungu ukadhihirike katika maisha yako hapa duniani. Dunia ione nuru ya Kristo ndani yako yeye unayeketi nae katika uzima wa milele. Wewe ni wathamani.

UZIMA NA MEMA YA MILELE

MAISHA YAKO YANAIFADHIWA NA MUNGU

MAISHA YAKO YANAIFADHIWA NA MUNGU Wakolosai 3:3-4 [3]Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. [4]Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Ukiwa unaamini katika Kristo Yesu na kazi aliyoikamilisha msalabani amini yakuwa Mungu ndiye pekee anayetunza maisha yako. Wewe ni zaidi ya ndege wa angani, wewe ni zaidi ya maua. Wewe ni wathamani.

KUENENDA KATIKA KRISTO

KUENENDA KATIKA KRISTO Wakolosai 2:6-7,9-10 [6]Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; [7]wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. [9]Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. [10]Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. Umekamilishwa ndani ya Kristo Yesu.

ENDELEA KUMWAMINI YESU KRISTO

Yohana 11:25-26 [25]Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; [26ye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? Yeye aliyefanyika dhambi ili sisi tupate uzima, nae aliimaliza dhambi kwa kifo cha msalaba na kutupa uzima wa milele pamoja nae katika ufufuko. Endelea kumuamini Kristo Yesu. Yeye ameyamaliza na kuyashinda yote. Siku njema

TUNAHESABIWA HAKI NDANI YA YESU

Warumi 6:5-6 [5]Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;6]mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; Hakika ndani ya Kristotunahesabiwa haki na hatuwi watumwa wa dhambi tena. Kristo Yesu amekwisha lipia yote kwa kupitia msalaba nasi tunapokea uzima tele kwa imani.

SALAMU ZA PASAKA

Salam Za Pasaka Wakolosai 2:13-15 [13]Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja ne, akiisha kutusamehe makosa yote; [14]akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwo tena, akaigongomea msalabani; [15]akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. Haleluya.