Skip to main content

Posts

SOMA BIBLIA MWENZANGU

Warumi 15:13

2018-09-01       Habari za asubuhi. Warumi 15:13 [13]Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, kaka nguvu za Roho Mtakatifu.  Ninaomba neno hili likafanyike hai na kuishi ndani yako kwa jina la Yesu mwezi huu ukasimamishwe imara katika yote Mungu aliyoyaweka mbele zako na ukaishi maisha yenye thamani na Utukufu wa Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.   Amina  Siku yako ni njema.  Shalom.
Recent posts

Luka 6:47-48

2018-05-12  Habari za asubuhi!  Luka 6:47-48 [47]Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. [48]Mfano wake ni mjengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.  Ninakuombea kwa Jina la Yesu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu uwe imara katika Imani yako kwa Kristo Yesu aliye mwamba  Shalom

NGUVU YA HEKIMA

Habari za asubuhi! Umeamshwaje! Na ndugu hapo wanaendeleaje? Mithali 24:3-4 [3]Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, [4]Na kwarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Roho wa Mungu akuangazie na kukupatia hekima kuyajenga yale yote yaliowekwa mikononi na moyoni mwako, ufahamu wake ulioko ndani yako ukathibitike na kwa maarifa yake akujaze na kuongeza thamani katika yote. Umebarikiwa. Shalom.

PENDO LA MUNGU

Wakolosai 1:12-13 [12]mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. [13]Nayetuokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; Mungu amethibitisha pendo lake kwako kupitia Kristo Yesu yeye aliye tustahilisha hata sasa kuyatenda yote yalio mbele zetu tukiwa na tumaini jema na mafanikio. Wewe ni wathamani.

WEWE NI WATHAMANI NDANI YA KRISTO

WEWE NI WATHAMANI NDANI YA KRISTO Waefeso 2:5-6 [5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja nKristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. [6]Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; Usisahau yaka umeketishwa pamoja na Kristo Yesu kwa ile imani uliyokuwa nayo ya Kumkiri Kristo Yesu ndani yako kuwa yeye ni Bwana na mokozi wa maisha yako. Shalom.

KUMTIZAMIA KRISTO YESU

KUMTIZAMIA KRISTO YESU. Waefeso 1:17 [17]Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; Ninakuombea Roho Mtakatifu akupe ufunuo kila unapojifunza kwa neno lake uweze kumfuata Kristo Yesu kwakua kila kitu kimewekwa chini yake. Siku yako ni njema.

UNAO UZIMA WA MILELE

UNAO UZIMA WA MILELE 1 Yohana 5:13 [13]Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jinla Mwana wa Mungu. ninakuombea Roho wa Mungu akufunulie kweli hii na Utukufu wa Mungu ukadhihirike katika maisha yako hapa duniani. Dunia ione nuru ya Kristo ndani yako yeye unayeketi nae katika uzima wa milele. Wewe ni wathamani.