Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2018

Warumi 15:13

2018-09-01       Habari za asubuhi. Warumi 15:13 [13]Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, kaka nguvu za Roho Mtakatifu.  Ninaomba neno hili likafanyike hai na kuishi ndani yako kwa jina la Yesu mwezi huu ukasimamishwe imara katika yote Mungu aliyoyaweka mbele zako na ukaishi maisha yenye thamani na Utukufu wa Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.   Amina  Siku yako ni njema.  Shalom.

Luka 6:47-48

2018-05-12  Habari za asubuhi!  Luka 6:47-48 [47]Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. [48]Mfano wake ni mjengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.  Ninakuombea kwa Jina la Yesu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu uwe imara katika Imani yako kwa Kristo Yesu aliye mwamba  Shalom